Shatt al Arab

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shat al Arab karibu na Basra
Ramani ya Shat al Arab karibu na Basra

Shat al Arab (Kiarabu: شط العرب shatt al arab "Mto Arabu") au kwa jina la Kiajemi Arvand Rud (اروندرود arvand rud "Mto Arvand") ni mto unaounganisha mito ya Hidekeli na Frati kabla ya kuishia katika Ghuba ya Uajemi.

Unaanza mahali nchini Irak ambako mito ya Hidekeli na Frati inaungana ukiendelea kwa kilomita 200 hadi baharini. Sehemu ya mwisho mto ni mpaka kati ya Irak na Uajemi.

Miji mikubwa kando la mto ni Basra upande wa Irak halafu Khorramshahr na Abadan upande wa Uajemi.