Nenda kwa yaliyomo

Shane & Shane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shane & Shane

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Shane Barnard,Shane Everett na Todd Cromwell
Aina ya muziki Nyimbo za Kikristo
Kazi yake Wanamuziki
Ala Gitaa
Tovuti Tovuti Rasmi


Shane & Shane ni bendi ya muziki ya Kikristo yenye makao yao Texas, Marekani. Inajulikana sana kwa nyimbo zao za sifa na za kuabudu. Bendi hiyo ina Shane Barnard (mwimbaji, mchezaji gitaa), Shane Everett (mwimbaji), Todd Cromwell (mchezaji gitaa ya bass, mwimbaji wa nyuma na Taylor Johnson (mchezaji gitaa la umeme). Meneja wa Shane & Shane ni Hunter Hall.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Shane Barnard

[hariri | hariri chanzo]

Ukristo ulichukua kipaumbele katika maisha ya Barnard alipokuwa katika daraja la tisa,alipoanza kuhudhuria kikundi cha vijana cha kanisa cha kibiblia. Alianza kuongoza ibada ya kuabudu,muda mfupi baada ya hapo. Katika mwaka alipokuwa mwanafunzi mdogo katika chuo kikuu cha Texas A&M, Barnard alianza kazi ya kurekodi.

Kabla ya kujiunga na Everett, Barnard alijiunga na rafiki yake Caleb Carruth{ na kutoa albamu. Albamu hiyo iliyoitwa Salvation Still Remainsilitolewa kwa idadi ndogo. Barnard na Carruth walisemekana kuwa walikuwa wamerekodi albamu hiyo kwa siku mbili kwa sababu walikuwa wakijilipia muda ya kurekodi katika studio na wakataka kutumia muda huo vizuri na kurekodi nyimbo nyingi. Familia na marafiki waliwaletea vinywaji na chakula walipokuwa studio. Barnard na,baadaye,Carruth walikubali kumaliza ushirkiano wao bila mgogoro, wakisema wanaelekea njia tofauti.

Shane alifunga ndoa na mwimbaji wa nyimbo za kisasa za Kikristo Bethany Dillon hapo mwaka wa 2008.

Shane Everett

[hariri | hariri chanzo]

Everett alizaliwa katika mji wa Dallas, Texas na baadaye akahamia Rowlett, kitongoji kilichokuwa karibu na hapo. Everett pia alisomea Chuo Kikuu cha Texas A & M. Usiku mmoja baada ya kucheza na bendi lake katika baa moja, Everett alipatwa na tukio lililomfanya ajue Mungu.Hii ilisababisha yeye kujiondoa katika bendi lake na akaanza kuhudhuria kanisa mara kwa mara.[1] Muda mfupi baada ya hayo, yeye alikutana na Barnard, na akawa akishiriki katika ibada ya wanafunzi ya kila wiki ya kusifu na kuabudu huko Texas A & M.

Bendi lilianza na Barnard akiimba akiwa pekee yake kisha Everett akaanza kujitokeza pia na kuchukua jukumu kubwa katika bendi. Walipotoa albamu yao ,ya 2003, Carry Away,bendi lilijulikana kirasmi kama Shane & Shane.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  • Rocks Won't Cry - 1998 (Shane Barnard, Independent)
  • Psalms - 2001 (Shane Barnard, Independent)
  • Window to the Inner Court - 2001 (Shane Everett)
  • Psalms - 2002 (Inpop)
  • Carry Away - 2003 (Inpop)
  • Upstairs - 2004 (Inpop)
  • Clean - 2004 (Inpop)
  • An Evening With Shane and Shane (CD/DVD) - 2005 (Inpop)
  • Bluegrass Sampler (akiwashirikisha. Peasall Sisters) - 2006 (Inpop)
  • Pages - 2007 (Inpop)
  • Glory in the Highest - 2008 (Inpop)
  • Everything Is Different - 2009 (Inpop)
  1. Shane Everett: Kugundua Mungu kwa Baa

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]