Seva mbadala
Seva mbadala (kwa Kiingereza: proxy server) ni seva ambayo inapatanisha ombi la wateja wa mtandao kwa seva nyingine. Kwa ufupi, huwa katikati na kazi yake ni kupatanisha wateja na wanachokihitaji.
Seva mbadala zilitengenezwa ili kuleta muundo mwafaka katika mifumo iliyosambazwa ya kompyuta (distributed computer systems). Leo hutumika sana kwa mitandao ili kuficha anwani ya IP ya mteja.
Matumizi ya seva mbadala
[hariri | hariri chanzo]- Ufuatiliaji na uchujaji - mashirika huhitaji kujua ni wavuti gani wanafanyakazi wanaingia na kuchuja zile ambazo wanaotumia mtandao wanatumia vibaya ama zile ambazo zinaonyesha picha za uchi na ngono. Hili laweza kufanyika kwa kutumia proxy server zitakazokusaidia kuchuja wavuti zisizo na faida kwa shirika.
- Kuchuja data iliyowekwa encryption
- Kuboresha utendaji - seva mbadala husaidia kufanya utendaji wa mitandao uwe na haraka zaidi.
- Kutafsiri
- Kufikia huduma bila kujulikana--unapotaka kutumia huduma kwa mitandao bila kujulikana, seva mbadala hukusaidia kuficha anwani yako ya IP ili uweze kufikia huduma zile bila ya kujulikana.
- Usalama - seva mbadala hukusaidia katika kuhakikisha kwamba u salama ukiwa kwa mitandao na kuwa manenosiri yako hayatochukuliwa na watu ambao hawafai. Mashirika pia huhitaji seva mbadala ili kuhakikisha kwamba seva zao hazitafikika kwa urahisi na wale wanaotaka kuyafikia kwa minajili baya (hackers).
Jinsi ya kuchagua seva mbadala itakayofaa
[hariri | hariri chanzo]Kasi ya utendaji
[hariri | hariri chanzo]Inafaa uchague seva mbadala ambayo ina kasi nzuri hivi kwamba inaweza kuwahudumia wateja wako kwa kasi nzuri wasije kuona kana kwamba mambo yatendeka polepole.
Nafasi ya kuhifadhi
[hariri | hariri chanzo]Seva mbadala yako iwe na nafasi kubwa ya kuhifadhi yale yote yaliyoko kwa seva na mitandao yako yote.
Usalama
[hariri | hariri chanzo]Seva yako lazima iwe ni salama isije ikaingiwa na kuibiwa manenosiri na hackers.
Mahala seva ilipo na kwenye seva yako ipo
[hariri | hariri chanzo]Ni vyema seva mbadala iwe mahala ambapo wateja watafikia huduma kwa urahisi yaani iwe karibu na nchi walioko.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |