Sertakonazoli
Sertakonazoli (Sertaconazole), inayouzwa kwa jina la chapa Ertaczo miongoni mwa zingine, ni dawa ya kuzuia fangasi inayotumika kutibu mguu wa mwanariadha, maambukizi ya fangasi yanayoambukiza sana kwenye ngozi au kichwani, maambukizi ya fangasi ya kawaida yanayosababisha mabaka madogo ya ngozi yaliyobadilika rangi, na maambukizi ya fangasi kwenye ngozi au utando telezi unaosababishwa na candida (candidiasis) ya ngozi.[1] Dawa hii inatumika kwa eneo la maambukizi mara mbili kwa siku kwa wiki nne.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na ngozi kavu, ngozi inayowaka na ngozi inayowasha.[1] Athari za mzio zinaweza kutokea.[1] Dawa hii ni katika kundi la madawa la azole.[1]
Sertakonazoli iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2003.[1] Nchini Marekani, bomba la gramu 60 hugharimu takriban dola 830 za Kimarekani kufikia mwaka wa 2021.[2] Hii inafanya kuwa ghali zaidi kuliko njia za kawaida na juu ya kaunta.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Sertaconazole Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 12 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Ertaczo Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 12 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Onion, Daniel K.; Glazer, James (25 Oktoba 2010). The Little Black Book of Primary Care (kwa Kiingereza). Jones & Bartlett Publishers. uk. 107. ISBN 978-1-4496-7197-6. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 12 Oktoba 2021.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sertakonazoli kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |