Nchi isiyo na dini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
     Nchi zisizo na dini rasmi      Nchi zilizo na dini rasmi      Utata au bila data

Nchi zisizo na dini (yaani zisizo na dini rasmi) ni nchi zilizoamua kutosimama upande wa dini yoyote kati ya zile zinazofuatwa na wakazi wake.[1]

Si kwamba nchi ya namna hiyo inapinga dini, bali inakusudia kuwatendea wakazi wote na miundo yao ya dini kwa usawa, bila upendeleo, ingawa pengine busara inadai kuzingatia wingi wa watu wanaozifuata, kwa mfano katika kukubali baadhi ya sikukuu katika kalenda ya taifa.

Kwa ajili hiyo siasa haitakiwi kutegemea dini yoyote, bali ustawi wa jamii unaolengwa kwa kuzingatia hoja ambazo nguvu yake inatokana na ukweli unaojulikana na akili tu.[2]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Temperman, Jeroen, State Religion Relationships and Human Rights Law: Towards a Right to Religiously Neutral Governance, BRILL, 2010, ISBN 9004181482