Sebene

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Sebene ni aina ya mapigo au midundo/ngoma tupu hasa hupigwa kwa kutumia gitaa na lina chembechembe za Rumba la Kikongo. Uanzishwaji wa sebene katika muziki wa Kongo hasa huhesabiwa kwa Franco Luambo na mpigaji gitaa maarufu wa Kikongo Plamedi Faustino, lakini inaonekana lilianza zamani na mpigaji gitaa mwingine wa Kikongo Henri Bowane ambaye huhesabiwa kwa heshima zote kama mwanzilishi halisi tangu katika miaka ya 1940.[1] Katika sebene, mpiga gitaa mmoja au zaidi hurudiarudia virai kadhaa, wakati mpiga solo hubuni maujanja ndani kibwagizo kikuu cha wimbo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Franco de Mi Amor, Robert Christgau, The Village Voice, July 3, 2001

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]