Nenda kwa yaliyomo

Sargramostim

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sargramostim, inayouzwa kwa jina la chapa Leukine, ni dawa inayotumika kuongeza seli nyeupe za damu kwa watu walio na viwango vyake vya chini au kabla ya utaratibu unaohusisha kuondolewa kwa seli nyeupe za damu kutoka kwenye damu (leukapheresis).[1] Dawa hii inatolewa kwa njia ya sindano ndani ya mshipa au chini ya ngozi.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na maumivu ya misuli.[1] Madhara yake mengine yanayoweza kutokea ni pamoja na kuongezeka kwa saratani, mzio mkali unaoweza kutishia maisha (anaphylaxis), upungufu wa kupumua na uvimbe.[1] Dawa hii ni recombinant granulocyte macrophage colony-stimulating factor (GM-CSF). [1]

Sargramostim iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1991.[1] Nchini Marekani mikrogramu 1,750 inagharimu takriban dola 2,000 za Marekani kufikia mwaka wa 2021.[2] Dawa hii imetengenezwa kutoka kwa chachu iliyobuniwa mahususi ya aina ya Saccharomyces cerevisiae.[1]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Sargramostim Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Agosti 2019. Iliwekwa mnamo 10 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Sargramostim Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 10 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sargramostim kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.