Nenda kwa yaliyomo

Sappho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kichwa cha sanamu cha Sappho.

Sappho (Kigiriki Σαπφώ sap-phō au Ψάπφω psap-phō; * kati ya 630 KK na 612 KK; † mnamo 570 KK)) alikuwa mshairi wa kike wakati wa ustaarabu wa Ugiriki ya Kale. Aliishi mjini Mytilene kwenye kisiwa cha Lesbos. Sehemu kubwa ya kazi zake zimepotea.

Alitunga shairi juu ya miungu na mapenzi. Nyakati za kale zilikusanywa katika vitabu tisa vilivyosafiwa na watu mashuhuri kama Plato na Horasi.

Alikusanya kundi la wanafunzi wa kike na kuwafundisha ushairi, muziki na uimbaji. Sehemu ya shairi na nyimbo zake ziliimbia mapenzi kati ya wanawake. Kwa hiyo lugha nyingi za Ulaya hutumia jina la kisiwa alipoishi kwa mapenzi kati ya wanawake (Kiing. "lesbian").

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sappho kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.