Sanamu ya Zeus mjini Olympia
Sanamu ya Zeus mjini Olympia ilimwonyesha mungu mkuu wa dini ya Ugiriki ya Kale. Zeus aliaminiwa kuwa baba wa miungu wa Ugiriki.
Sanamu yenye kimo cha mita 12 ilimwonyesha mungu huyu akikalia kitini kama mzee mwenye hekima. Ilikaa kwenye hekalu kubwa ya Zeus ya Olympia kando la uwanja wa michezo ya Olimpiki. Ilitengenezwa na mchongaji mashuhuru Phidias aliyejenga kiini cha ubao na chuma pamoja na jasi na kuifunika kwa ubao, dhahabu na pembe. Phidias aliifanyia kazi kwa miaka 8 kuanzia mwaka 438 KK. Baada ya kuimaliza Phidias alishtakiwa kuwa ameiba kiasi cha dhahabu iliyokusudiwa kwa sanamu akauawa.
Watu wa Kale walihesabu sanamu hii kati ya maajabu saba za dunia.
Mwaka 40 BK Kaisari wa Roma Caligula alishindwa kupeleka sanamu kwenda mjini Roma. Lakini wakati wa karne ya 4 ilipelekwa Konstantinopoli ikasimamishwa pale hadi mwaka 475 ilipoharibiwa katika moto kubwa.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- "The Statue of Zeus at Olympia" Ilihifadhiwa 22 Januari 2009 kwenye Wayback Machine.
- Colin Delaney, "A Wonder to Behold: The Statue of Olympian Zeus" Ilihifadhiwa 4 Mei 2006 kwenye Wayback Machine.
- Archaeopaedia: Statue of Zeus Ilihifadhiwa 5 Februari 2007 kwenye Wayback Machine. With bibliography
- (Ellen Papakyriakou) Olympia: Art: the chryselephantine statue of Zeus
- Michael Lahanas, "The colossal Zeus statue of Pheidias" Ilihifadhiwa 3 Aprili 2013 kwenye Wayback Machine.
- David Fenzl "Recreating Olympic Statuary" Archived 2008-12-20 at Archive.today