Samuel García

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
García mnamo 2017
García mnamo 2017

Samuel Garcia Cabrera (alizaliwa 4 Desemba 1991) ni mwanariadha wa Hisipania aliyejikita kwenye mbio ya mita 400.[1] Aliliwakilisha taifa lake kwenye mbio fupi za mita 4 x 400 kwenye Mashindano ya Ubingwa wa Dunia mwaka 2013 na alishinda medali ya Shaba kwenye Mashindano ya Ubingwa wa Ulaya mwaka 2018. Mafanikio yake bora mpaka sasa ni nafasi ya saba kwenye Ubingwa wa Ulaya 2014.

Rekodi yake bora kwenye mita 400 ni sekunde 45.00 nje(Monachil 7 Julai 2017) na sekunde 46.35 ndani (Salamanca 2017).  

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Samuel GARCÍA | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-16.