Ryan Gravenberch

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ryan Gravenberch akiicheze FC Bayern München mwaka 2022
Ryan Gravenberch
Nchi Bendera ya Uholanzi Uholanzi
Kazi yake Mchezaji wa soka
Cheo Mchezaji


Ryan Jiro Gravenberch (alizaliwa 16 Mei 2002) ni mchezaji wa soka wa Uholanzi ambaye anacheza kama kiungo wa kati wa klabu ya Liverpool ya Ligi Kuu ya Uingereza na timu ya taifa ya Uholanzi.

Maisha yake ya Klabu[hariri | hariri chanzo]

Ajax[hariri | hariri chanzo]

Gravenberch alijiunga na klabu ya vijana ya Ajax(Ajax Youth Academy) mwaka 2010, na kujitahidi hadi kupanda kati nafasi za juu.[1] Mnamo tarehe 7 Juni 2018, alipata tuzo yake ya kwanza ya Abdelhak Nouri, amabayo ilikuwa ikidhihirisha kiwango bora katika akademi ya Ajax.[2] Alitia saini mkataba wake wa kwanza wa kikazi na Ajax siku hiyo hiyo, ukimuweka klabuni hapo hadi 2023.[3] Gravenberch alicheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa akiwa na Jong Ajax katika ushindi wa 5-2 katika ligi ya Eerste Divisie dhidi ya FC Dordrecht mnamo 24 Agosti 2018..[4]

Gravenberch alicheza mechi yake ya kwanza na Ajax mnamo 23 Septemba 2018,wakipoteza kwa kichapo cha 3-0 Eredivisie dhidi ya PSV Eindhoven..[5] Gravenberch amekuwa mchezaji mdogo zaidi wa Ajax kucheza Eredivisie akiwa na miaka 16 na siku 130, akiipita rekodi ya miaka 16 na siku 242 iliyowekwa na Clarence Seedorf.[6]

Mnamo tarehe 25 Novemba 2020, Gravenberch alifunga bao lake la kwanza la UEFA Champions League katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Midtjylland FC msimu wa 2020-21.[7]

Tarehe 18 Aprili 2021, Gravenberch alifunga bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya SBV Vitesse katika Fainali ya Kombe la KNVB la 2021.[8]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Toptalent Ryan Gravenberch uit Zuidoost tekent bij Ajax - Bijlmer en Meer". 10 July 2018.  Check date values in: |date= (help)
  2. "Ajax renames talent award after Abdelhak Nouri". 8 June 2018.  Check date values in: |date= (help)
  3. "Gravenberch and Brobbey sign first Ajax contracts - Football Oranje". 7 June 2018. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-23. Iliwekwa mnamo 2023-11-01.  Check date values in: |date= (help)
  4. "Ajax II vs. Dordrecht - 24 August 2018 - Soccerway". Soccerway. 
  5. "PSV vs. Ajax - 23 September 2018 - Soccerway". Soccerway. 
  6. "Cookies op gelderlander.nl - gelderlander.nl". www.gelderlander.nl. 
  7. "Ajax 3–1 Midtjylland". UEFA. 25 November 2020.  Check date values in: |date= (help)
  8. "Neres’ stoppage-time goal seals Dutch Cup win", AFC Ajax, 18 April 2021. 
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ryan Gravenberch kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.