Rosebud Kurwijila
Rosebud Kurwijila | |
Amezaliwa | Tanzania |
---|---|
Nchi | Tanzania |
Kazi yake | Mkuu wa Idara ya uchumi wa vijijini na Kilimo |
Rosebud Violet Kurwijila, wa Tanzania, ni mkuu wa idara ya maendeleo ya kiuchumi vijijini na kilimo ya Umoja wa Afrika. Kabla alikua ni mratibu wa programu ya maendeleo ya ACTIONAID iliyopo Tanzania.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Rosebud Kurwijila, ni mtanzania na ni mkuu wa idara ya uchumi wa vijijini na kilimo. Rosebud alipata shahada ya kwanza ya kilimo kutoka katika chuo cha kilimo cha Sokoine University of Agriculture, kilichopo nchini Tanzania mnamo mwaka 1976, mwaka 1983 alipata shahada ya uzamili ya uchumi wa kilimo kutoka chuo kikuu cha London University of London na pia shahada ya uzamili ya falsafa katika uchumi na maendeleo mwaka 1994 kutoka katika chuo cha East Anglia (UK) (1994).
Katika kipindi chake cha ajira ameshawahi kutumika kama mshauri katika sehemu tofauti zinazohusiana na mambo ya kilimo, uchumi wa vijijini na usalama wa chakula. Mwaka 1995 – 1997, alikua ni mshauri mwandamizi kutoka katika kampuni inayohusika na huduma ya ushauri, alihusika na upatikanaji na ufanyaji wa miradi.
Rosebud amechapisha makala nyingi katika majarida ya kimataifa kuhusu usalama wa chakula, uchumi wa vijijini, teknolojia ya kilimo na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Maeneo yake ya ufanisi ni pamoja na usimamizi wa mipango, utungaji wa sera na usimamizi wa wafanyakazi.
Ameolewa na pia ana watoto wanne (4).[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-27. Iliwekwa mnamo 2018-06-20.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Rosebud Kurwijila bio Ilihifadhiwa 27 Septemba 2011 kwenye Wayback Machine.
- Tovuti ya Bunge la Tanzania
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |