Ron Kenoly

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ron Kenoly (alizaliwa tarehe 6 Desemba, 1944 huko Coffeyville, Kansas) ni kiongozi wa ibada ya Kikristo, mwimbaji na mtunzi ambaye tume yake ni "kujenga mazingira ya kuweka wazi uwepo wa Mungu". Mtindo wa muziki wake ni wa sifa za kufurahisha na umahiri katika utumizi wa ala. Ingawa Kenoly hucheza mwenyewe katika rekodi yake moja tu, yeye huongoza mnamo kwa sauti yake na daima na husaidiwa na wanamuziki na kwaya kubwa.

Yeye ana digrii kadhaa, ikiwa ni pamoja na shahada ya muziki kutoka Alameda College, digrii ya 'Master' kutoka Faith Bible College, na 'Doctorate' ya Huduma katika Muziki wa Dini kutoka Friends International Christian University. [1] taaluma yake ya muziki ilianza baada ya muda alipokuwa katika kundi la wanajeshi wa Angani Marekani. [1] awali alikuwa na kundi inayoitwa Shades of Difference (Vivuli vya Mabadiliko), lakini masuala ya familia yake yakamsababisha kukihama kikundi. Mafanikio yake makuu yalikuwa katika mwaka wa 1992 ambapo Lift Him Up ilipokuwa albamu iliyouza zaidi kwa kiasi hicho. [1] Welcome Home pia ilipata umaarufu mkuu, na kwa mujibu wa Billboard ilikuwa miongoni mwa zile bora kwenye "Top Indie Contemporary Christian Music album", [1] na kushinda tuzo la Chama cha Nyimbo za Injili cha DOVE katika "Albamu ya Sifa na Kuabudu" mnamo mwaka 1997. [2] Alisajiliwa katika "Integrity Music" lakini hivi sasa hafanyi kazi ya kuwarekodia tena.

Alianza kufanya kazi katika huduma kamili mnamo mwaka 1985. Alianza kama kiongozi wa ibada katika Jubilee Christian Centre mjini San Jose, California. Si muda mrefu baadaye, mwaka 1987, alikadiriwa kuwa Mchungaji wa muziki. Kama kiongozi wa ibada, lengo lake kuu lilikuwa kuongoza ibada. Alipokuwa Mchungaji, akawa mchungaji mkuu katika idara nzima ya muziki ya Jubilee Christian Centre. Mwaka 1993, baada ya mafanikio ya rekodi mbili za Integrity, alianza kupokea mialiko kutoka kote duniani. Makanisa yalimtaka kuja kuongoza sifa na ibada, na pia kuwasaidia kuendeleza idara zao za muziki. Hivyo muda mfupi baadaye, aliitwa Balozi wa muziki katika Jubilee Christian Centre. Alitumwa na kanisa kama balozi duniani ili kusaidia kuendeleza makanisa na kupata uwiano kati ya ibada na Neno. Mwaka 1996, alipokea shahada ya 'Doctorate' katika Huduma ya Muziki wa Kidini. Mwaka 1999, alipata wito kuhama kutoka California na kuelekea Pwani ya Mashariki (East Coast). Kwa hivyo, alihamisha huduma hadi Central Florida ambapo anaendelea kusafiri, kuzungumza, kuimba na kufundisha na kurekodi. Yeye anaimba ulimwenguni kote.

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ron Kenoly kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.