Robin Sharma
Robin Sharma ni mwandishi kutoka nchini Kanada, anayejulikana zaidi kwa kitabu chake mashuhuri sana kiitwacho The Monk Who Sold His Ferrari . [1] Sharma alifanya kazi za sheria kama wakili wa kesi hadi alipofikisha umri wa miaka 25, [2] pindi alipochapisha mwenyewe kitabu kiitwacho MegaLiving (1994), kitabu kuhusu mafadhaiko na hali ya kiroho. [3] Hapo awali alichapisha pia The Monk Who Sold His Ferrari, ambacho kilichukua nafasi kubwa katika usambazaji wake na kampuni ya HarperCollins . [1] Sharma amechapisha vitabu vingine 12, na kuanzisha kampuni ya mafunzo ya Sharma Leadership International. [4]
Maisha ya awali na kazi
[hariri | hariri chanzo]Sharma ni mwenye asili ya Kihindi. Ana Shahada ya Uzamili ya Sheria. Hapo awali, alifanya kazi kama wakili, lakini anasema hakuweza kupata kuridhika au amani ya ndani pindi alipokuwa akifanya kazi hio. Sharma alianza kazi yake ya uandishi akiwa na umri wa miaka 25. Alijulikana sana kwa kitabu chake cha pili,The Monk Who Sold His Ferrari . Baada ya kitabu chake cha pili kufanikiwa, aliacha kazi yake ya uwakili na kuwa mwandishi wa wakati wote. Baadaye, pia alianza kuzungumza mbele ya watu katika majukwa tofauti tofauti na akawa maarufu kama mzungumzaji. Anashauriwa na kupewa mafunzo mbalimbali na Wakurugenzi na viongozi tofauti tofauti kutoka ulimwenguni na hivyo kupata ushauri wa jinsi ya kuwaweka wafanyakazi wao katika hali itakayo wapa motisha katika maisha yao ya kazi na maisha ya kujitambua na kujijua zaidi, kwa hakika kwayo ndipo mafanikio yalipo. Pia amefanya mafunzo kutoka kwenye makampuni mengine mengi, kama vile Nike, Microsoft, IBM, na FedEx . Mashirika mengin kama vile Chuo Kikuu cha Yale, Shule ya Biashara ya Harvard, na NASA pia humwita kutoa hotuba kwa umma.
Baadhi ya machapisho
[hariri | hariri chanzo]- Megaliving!: 30 Days to a Perfect Life (1994, ISBN 978-8172246143)[3]
- '[The Monk Who Sold His Ferrari (1997, ISBN 978-8179-921623)
- Leadership Wisdom from the Monk Who Sold His Ferrari (1998, ISBN 978-1401905460)[5]
- Who Will Cry When You Die: Life Lessons from the Monk Who Sold His Ferrari (1999, ISBN 978-8179922323)[5]
- Family Wisdom from the Monk Who Sold His Ferrari (2001, ISBN 978-1401900144)
- The Saint, the Surfer, and the CEO (2002, ISBN 978-1401900168)
- The Greatness Guide: 101 Lessons for Making What's Good at Work and in Life Even Better (2006, ISBN 978-0061238574)[6]
- The Greatness Guide Book 2: 101 More Insights to Get You to World Class (2008, ISBN 978-1554684038)
- The Leader Who Had No Title (2010, ISBN 978-1439109137)[7]
- The Secret Letters of the Monk Who Sold His Ferrari (2011, ISBN 978-0007321117)[4]
- Little Black Book for Stunning Success (2016, ISBN 9788184959895)
- The 5 AM Club (2018, ISBN 978-1443456623)
- The Everyday Hero Manifesto (2021, ISBN 9781443456647)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Why millions go to this man for advice; Robin Sharma offers simple rules to live by. The hard part is living up to them every day". Victoria Times-Colonist, November 29, 2011.
- ↑ "Spiritual fable sheds light on life's big questions; Sharma's Seven Secrets". Edmonton Journal, September 23, 1997.
- ↑ 3.0 3.1 "Toward a healthy lifestyle East Meets West: Meditation and yoga can be used by anyone". The Globe and Mail, March 3, 1995.
- ↑ 4.0 4.1 "Sharma shows the way: Novel maps out road to happiness". Toronto Star, November 5, 2011.
- ↑ 5.0 5.1 "Marketing a message: Self-publishing takes time, money, commitment". Calgary Herald, May 16, 1999.
- ↑ "In the marathon of life, some wisdom bites to help the cause". The Globe and Mail, June 21, 2006.
- ↑ "Leaders Without Titles". The Globe and Mail, March 31, 2010.