Nenda kwa yaliyomo

Resego Kgosidintsi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Resego Natalie Kgosidintsi[1] ni mwanaharakati wa haki za wanawake na mgombea wa kisiasa kutoka Botswana. Katika shughuli za kisiasa, anajulikana kama Petrol Bomb kwa imani zake za kisiasa zilizo wazi.[2][3][4]

Maisha na Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Resego Kgosidintsi ni binti wa Bontsibokae na Colline Kgosidintsi,[2] aliyezaliwa kijijini Serowe, Botswana.[1] Akiwa mtoto, alishiriki katika timu zamdahalo wa shule, akisafiri kwenda Ghana na Zimbabwe. Alisoma sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Botswana. Alipokuwa chuoni, Kgosidintsi alihudumu kama Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi, na alikuwa mwenyekiti wa kwanza mwanamke wa Harakati Dhidi ya Kudhibiti Wanafunzi.[2]

Kgosidintsi amejulikana kwa msimamo wake wa moja kwa moja katika kupinga ukatili dhidi ya wanawake.Kisiasa, ameunga mkono chama cha Botswana National Front kinacho ongozwa na Duma Boko.Anajitambulisha kama mwanaharakati wa haki za wanawake na anaunga mkono kuhalalishwa kwa kazi ya ngono.[5]Pia ameshiriki kuhamasisha wanawake kugombea nafasi za kisiasa kutokana na ukosefu wa usawa wa kijinsia katika vyombo vya siasa nchini Botswana, akilenga kuona mwanamke anagombea kila nafasi ya uongozi katika uchaguzi mkuu wa Botswana wa mwaka 2024.

Kgosidintsi alikuwa Katibu wa Kata ya Kijiji na mweka Hazina wa Gaborone Central, kisha akachaguliwa kuwa mjumbe wa nyongeza wa Kanda ya Kusini–Kati wa chama cha Botswana National Front.Baadae alihudumu kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho.Mwaka 2020, alikamatwa na kuachiwa siku iliyofuata, jambo lililosababisha ukosoaji dhidi ya serikali kwa kukamata wanachama wa upinzani[6].Kgosidintsi aligombea urais wa Umoja wa Vijana wa Botswana National Front mwaka 2020.Uchaguzi huo uliahirishwa hadi mwaka 2022, ambapo alimshinda mpinzani wake Carter Joseph kwa kura 337 dhidi ya 26[7].Pia aligombea kiti cha Ubunge cha jimbo la Gaborone Bonnington North mwaka 2022.Mwezi Oktoba 2022, alizua mjadala baada ya kukosoa hadharani uongozi wa vyama vya upinzani kwa kushindwa kukiondoa chama tawala madarakani.

  1. 1 2 Kgosidintsi, Resego Natalie (2017). "Student Activism and Youth Agency in Botswana". Buwa! (8): 34–40.
  2. 1 2 3 Kolantsho, Neo (2020-11-25). "Resego Unplugged". The Midweek Sun.
  3. Shaya (2022-09-27). "Chillin' out Friday 23 September 2022". TheVoiceBW.
  4. "Kgosidintsi steers BNFYL". Africa Press (kwa American English). 2022-05-31. Iliwekwa mnamo 2023-02-24.
  5. Thalefang Charles (2020-02-10). "Legalise Sex Work - Kgosidintsi". Mmegi Online (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-02-16.
  6. "Botswana's govt accused of arresting opposition members, journalists", eNCA (kwa Kiingereza), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-02-24, iliwekwa mnamo 2026-02-16
  7. cfeditoren (2022-05-31). "Kgosidintsi steers BNFYL". Botswana (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-02-16.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Resego Kgosidintsi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.