Msogeo mwekundu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Redshift)

Msogeo mwekundu (ing. redshift) ni istilahi ya lugha ya fizikia kutaja maongezeko katika urefu wa mawimbi sambamba na kupungua kwa marudio, nishati ya fotoni na mnururisho sumakumeme kama mwanga. Mabadiliko ya kinyume yaani kupungua kwa urefu wa wimbi na kuongezeka kwa marudio na nishati hujulikana kama msogeo mwekundu hasi, au msogeo buluu (blueshift). Majina hayo hutokana na rangi nyekundu na buluu ambayo huunda sehemu mbili za mwisho wa spektra ya nuru inayoonekana.

Msogeo mwekundu na buluu ni matokeo ya athari ya Doppler kwa nuru na mawimbi ya sumakuumeme kwa jumla. Utafiti wake ni muhimu hasa katika fani ya astronomia. Hapa inawezesha kukadiria umbali na kasi kwa violwa vya anga vya mbali.

Wanaastroomia huangalia hapa mistari ndani ya spektra inayoonyesha ni elementi gani inayopatikana kwenye nyota ambayo ni asili ya nuru inayopimwa. Elementi hizo zinaleta ruwaza ya pekee ya mistari ndani ya spektra ambayo ni sawa kote ulimwenguni. Lakini kama chanzo cha nuru kina mwendo kwenda mbali na mtazamazi, ruwaza hiyo imesogezwa upande.

  1. Mawimbi husafiri kati ya vitu ambavyo vinasonga mbali (" relativistic " redshift, mfano wa athari ya Doppler inayohusiana )
  2. Mionzi husafiri kuelekea kitu katika kuwa uwezo mvuto, yaani kuelekea kitu katika chini sana curved (flatter) spacetime ( mvuto redshift )
  3. Mionzi husafiri kupitia nafasi ya kupanua ( redshift cosmological ). Uchunguzi kwamba vyanzo vyote vya taa vya mbali vya kutosha vinaonyesha redshift inayolingana na umbali wao kutoka Dunia inajulikana kama sheria ya Hubble .
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Msogeo mwekundu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.