Nenda kwa yaliyomo

Rabiu Afolabi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rabiu Afolabi

Rabiu Afolabi (alizaliwa 18 Aprili 1980) ni mchezaji wa zamani wa soka wa Nigeria, ambaye alikuwa akicheza kama beki wa kati.

Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Afolabi alichangia nafi kubwa katika Michuano ya Vijana ya Afrika 1999, akifunga mabao mawili dhidi ya Cameroon katika nusu fainali. Nigeria hatimaye ilimaliza katika nafasi ya pili katika mashindano baada ya kupoteza 0-1 dhidi ya wenyeji, Ghana, katika fainali.

Baadaye, alikuwa nahodha wa timu ya Nigeria chini ya miaka 20 katika Kombe la Dunia la Vijana la FIFA 1999 nchini Nigeria.

Tarehe 17 Juni 2000, Afolabi alicheza rasmi kabisa katika timu ya taifa ya Nigeria katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia 2002 dhidi ya Sierra Leone. Alikuwa sehemu ya kikosi cha Nigeria katika Kombe la Dunia 2002 na Kombe la Dunia 2010.

Uchezaji

[hariri | hariri chanzo]

Afolabi ni beki imara na mrefu, ambaye anajua kucheza katika nafasi yake vizuuri. Pia ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa pembeni au kiungo wa ulinzi. Katika mashambulizi, ni hatari kwenye mipira ya kuotea.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rabiu Afolabi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.