Nenda kwa yaliyomo

Qamar Aden Ali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Qamar Aden Ali (Kisomali: Qamar Aadan Cali‎, Kiarabu: قمر آدم علي‎; 19 Septemba 1957 – 3 Desemba 2009) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa. Aliuawa wakati akihudumu kama Waziri wa Afya katika serikali ya Mpito ya Shirikisho la Somalia.

Qamar alizaliwa tarehe 19 septemba 1957 katika kijiji kidogo nje ya Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.Alikuwa mtoto wa tatu (3) kati ya watoto 11. Qamar alikulia huko Mogadishu ambapo pia alienda shule na kuhitimu chuo. Baadaye alihamia Ujerumani Mashariki kusomea Sayansi ya siasa na baadaye akasoma sheria nchini Uingereza. Hatimaye alihitimu kuwa mwanasheria na akawa raia wa Uiengereza. Katikati ya miaka ya 1990, Qamar alirudi Somali , ambako baadaye alijiunga na serikali ya mpito ya taifa hilo.. Kuanzia 2007 hadi kifo chake, alihudumu kama Waziri wa afya wa kitaifa.[1]

Kuna shule iliyopewa jina kwa heshima yake na hii ingefanyiwa ukarabati mwaka wa 2018 kama ilivyotangazwa na Waziri wa Somalia Deqa Yasin mnamo Novemba 2018.[2]

  1. Shah, Allie. "Minneapolis surgeon feels calling back to Somalia", Star Tribune, December 19, 2009. 
  2. AMISOM Public Information (2018-11-24), 2018_11_24_Qamar_School_Rehabilitation-23, iliwekwa mnamo 2020-03-18