Proxy server

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Proxy server ni seva ambayo inapatanisha ombi la wateja wa mtandao kwa seva nyingine. Kwa ufupi, huwa katikati na kazi yake ni kupatanisha wateja na wanachokihitaji.

Proxy server zilitengenezwa ili kuleta muundo mwafaka katika mifumo iliyosambazwa ya kompyuta (distributed computer systems). Leo proxy server hutumika sana kwa mitandao ili kuficha anwani ya IP ya mteja.

Matumizi ya proxy server[hariri | hariri chanzo]

  • Ufuatiliaji na uchujaji - mashirika huhitaji kujua ni wavuti gani wanafanyakazi wanaingia na kuchuja zile ambazo wanaotumia mtandao wanatumia vibaya ama zile ambazo zinaonyesha picha za uchi na ngono. Hili laweza kufanyika kwa kutumia proxy server zitakazokusaidia kuchuja wavuti zisizo na faida kwa shirika.
  • Kuchuja data iliyowekwa encryption
  • Kuboresha utendaji - proxy server husaidia kufanya utendaji wa mitandao uwe na haraka zaidi.
  • Kutafsiri
  • Kufikia huduma bila kujulikana--unapotaka kutumia huduma kwa mitandao bila kujulikana, proxy server hukusaidia kuficha anwani yako ya IP ili uweze kufikia huduma zile bila ya kujulikana.
  • Usalama - proxy server hukusaidia katika kuhakikisha kwamba u salama ukiwa kwa mitandao na kuwa manenosiri yako hayatochukuliwa na watu ambao hawafai. Mashirika pia huhitaji proxy server ili kuhakikisha kwamba seva zao hazitafikika kwa urahisi na wale wanaotaka kuyafikia kwa minajili baya (hackers).

Jinsi ya kuchagua proxy server itakayofaa[hariri | hariri chanzo]

Kasi ya utendaji[hariri | hariri chanzo]

Inafaa uchague proxy server ambayo ina kasi nzuri hivi kwamba inaweza kuwahudumia wateja wako kwa kasi nzuri wasije kuona kana kwamba mambo yatendeka polepole.

Nafasi ya kuhifadhi[hariri | hariri chanzo]

Proxy server yako iwe na nafasi kubwa ya kuhifadhi yale yote yaliyoko kwa seva na mitandao yako yote.

Usalama[hariri | hariri chanzo]

Seva yako lazima iwe ni salama isije ikaingiwa na kuibiwa manenosiri na hackers.

Mahala seva ilipo na kwenye seva yako ipo[hariri | hariri chanzo]

Ni vyema proxy server iwe mahala ambapo wateja watafikia huduma kwa urahisi yaani iwe karibu na nchi walioko.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]