Nenda kwa yaliyomo

Propanthelini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

 Propanthelini (Propantheline) ni dawa inayotumika kutibu kutokwa na jasho kupindukia, ugonjwa kuumwa tumbo na matumbo, na kupoteza udhibiti wa kibofu.[1] Imekuwa ikitumika kwa ugonjwa wa kidonda cha peptiki; hata hivyo ushahidi wa kuunga mkono matumizi haya ni duni.[2] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kinywa kikavu na uoni wenye ukungu.[2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha mapigo ya moyo yasiyo mazuri (arrhythmias), mzio mkali unaoweza kutishia maisha (anaphylaxis), na kuhisi usingizi.[1][2] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[2] Dawa hii ni ya aina ya antimuscarinic.[2]

Propanthelini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1953.[2] Nchini Uingereza, vidonge 112 vya miligramu 15 uligharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £20 mwaka wa 2021.[1] Nchini Marekani, kiasi hiki kinagharimu takriban dola 300 za Kimarekani.[3]

  1. 1.0 1.1 1.2 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 94. ISBN 978-0857114105.
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 "Propantheline Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Propantheline Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Propanthelini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.