Nenda kwa yaliyomo

Polidokanoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Polidokanoli (Polidocanol), inayouzwa kwa jina la chapa Asclera, ni dawa inayotumika kutibu mishipa iliyovimba hasa kwenye (varicose veins) ikiwa ni pamoja na mishipa ya midogo ya damu iliyopanuliwa (spider veins) na mishipa inayoonekana chini ya ngozi yako yenye rangi ya bluu-zambarau (reticular veins). [1] Dawa hii inaweza pia kutumika kwa ugonjwa wa ukuaji unaotokana na mishipa ya ziada ya damu kwenye ngozi (hemangiomas), na ulemavu wa mishipa.[2] Inatolewa kwa njia ya sindano kwenye mshipa kama sehemu ya matibabu ya ugonjwa wa mishipa ya miguu (sclerotherapy).[3]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na athari ndogo ya ndani.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha mzio mkali unaoweza kutishia maisha (anaphylaxis), kuganda kwa damu, na kufa wa seli au tishu kupitia ugonjwa au jeraha (tissue necrosis).[1] Ni sabuni za kikundi cha nonionic.[3]

Polidokanoli iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2010.[1] Nchini Marekani, mililita 2 za kioevu chake zinagharimu takriban dola 22 za Marekani kufikia mwaka wa 2021. [4] Pia hutumiwa kwa njia maalumu katika vipodozi.[5]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "DailyMed - ASCLERA- polidocanol injection, solution". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Gao Z, Zhang Y, Li W, Shi C (Januari 2018). "Effectiveness and safety of polidocanol for the treatment of hemangiomas and vascular malformations: A meta-analysis". Dermatologic Therapy. 31 (1). doi:10.1111/dth.12568. PMID 29082587.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 "Polidocanol Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Mei 2016. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Asclera Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "ADDENDUM to the SCCP opinion on polidocanol (SCCP/1130/07)" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 14 Juni 2015. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Polidokanoli kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.