Pegaptanib
Jina la Utaratibu la (IUPAC) | |
---|---|
RNA, ((2'-deoxy-2'-fluoro)C-Gm-Gm-A-A-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-(2'-deoxy-2'-fluoro)C-Am-Gm-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-Gm-Am-Am-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-Gm-(2'-deoxy-2'-fluoro)C-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-(2'-deoxy-2'fluoro)U-Am-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-Am-(2'-deoxy-2'-fluoro)C-Am-(2'-deoxy-2'-fluoro)U-(2'deoxy-2'-fluoro)C-(2'-deoxy-2'-fluoro)C-Gm-(3'→3')-dT), 5'-ester with α,α'-[4,12-dioxo-6[[[5-(phosphoonoxy)pentyl]amino]carbonyl]-3,13-dioxa-5,11-diaza-1,15-pentadecanediyl]bis[ω-methoxypoly(oxy-1,2-ethanediyl)], sodium salt[1] | |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Macugen |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
MedlinePlus | a607057 |
Kategoria ya ujauzito | B(US) |
Hali ya kisheria | ? (US) |
Njia mbalimbali za matumizi | Sindano ya ndani ya vitreous (substansi inayofanana na geli ndani ya jicho) |
Data ya utendakazi | |
Nusu uhai | Siku kumi |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C294H342F13N107Na28O188P28[C2H4O](m+n) (m+n≈900) |
Massi ya molekuli | ~50 kg/mol |
(Hiki ni nini?) (thibitisha) |
Pegaptanib, inayouzwa kwa jina la chapa Macugen, ni dawa iliyotumika kutibu ugonjwa wa kuzorota kwa sehemu ya kati ya retina unaohusiana na umri na unaosababisha unyevunyevu (AMD).[2] Ilitumiwa kwa kudunga sindano kwenye jicho.[2]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kutoona vizuri, ukungu kwenye lenzi ya jicho, ambayo inaweza kusababisha upungufu wa kuona (ugonjwa wa mtoto wa jicho), kuvuja damu kwenye utando wa jicho, maumivu ya macho na kuongezeka kwa shinikizo la ndani ya jicho.[3] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha shambulio la mzio mkali (anaphylaxis) na maambukizi ya ndani ya jicho (endophthalmitis).[3] Dawa hii inafanya kazi kwa kuzuia sababu ya ukuaji wa mishipa ya endothelial (VEGF).[3]
Pegaptanib iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya matibabu nchini Marekani mwaka wa 2004.[4] Ingawa iliidhinishwa barani Ulaya mnamo mwaka wa 2006, idhini hii iliondolewa.[5] Nchini Marekani, chupa ya miligramu 0.3 inagharimu takriban dola 780 za Kimarekani. [6] Kufikia mwaka wa 2016, haikuwa ikipatikana tena nchini Marekani.[7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Drug Information: Pegaptanib Sodium Injection Archived 2013-12-14 at the Wayback Machine
- ↑ 2.0 2.1 "Macugen (pegaptanib)" (PDF). European Medicines Agency: 1–3. 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-12-13. Iliwekwa mnamo 2013-12-08.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 "Pegaptanib Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "MACUGEN- pegaptanib sodium injection, solution". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Macugen". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Macugen Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Wong, Randall (2016). "Ocular drug delivery systems" (PDF). Retina Today. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 26 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 26 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)