Nenda kwa yaliyomo

Patrick Ndakidemi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Patrick Ndakidemi
Amezaliwa22 Julai 1956
UtaifaMtanzania
Kazi yakeProfesa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Mbunge wa Moshi vijijini

Patrick Alois Ndakidemi (kuzaliwa 22 Julai 1956) ni profesa wa sayansi za kilimo kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.[1] Ndakidemi ni mbobezi wa masuala ya afya ya mimea kwenye udongo duni pamoja. [2]

Kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini tangu mwaka 2020. Pia ni mwenyekiti wa kamati ya kilimo, mifugo na maji ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[3][4][5]

Profesa Ndakidemi ana shahada ya uzamili kutoka chuo cha Cape Peninsula aliyopata mwaka 2006. Kabla ya hapo alifanya shahada ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mwaka 1992 ambapo ndipo alipopata shahada ya kwanza mwaka 1987. Mwaka 1990 alifanikiwa kupata stashahada ya juu kutoka Agriculture University of Norway. [6]

Kabla ya elimu ya juu, alisoma shule ya msingi Singachini na shule ya sekondari Kibo. [7]

  1. "NM-AIST website". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-12-31. Iliwekwa mnamo 2023-12-31. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |name= ignored (help)
  2. "Google scholar". {{cite web}}: Unknown parameter |name= ignored (help)
  3. "Parliament of Tanzania". {{cite web}}: Unknown parameter |name= ignored (help)
  4. "MUWSA website". {{cite web}}: Unknown parameter |name= ignored (help)
  5. "Mwananchi newspaper website". {{cite web}}: Unknown parameter |name= ignored (help)
  6. "Parliament of Tanzania". {{cite web}}: Unknown parameter |name= ignored (help)
  7. "Parliament of Tanzania". {{cite web}}: Unknown parameter |name= ignored (help)
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Patrick Ndakidemi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.