Pafolasianini
Pafolasianini (Pafolacianine), inayouzwa chini ya jina la chapa Cytalux, ni ajenti ya kupiga picha inayotumika katika upasuaji unaoongozwa na rangi zenye kuakisi mwanga (fluorescence-guided surgery).[1] Hasa hutumiwa kupata maeneo ya saratani ya ovari.[1] Dawa hii inatolewa kwa njia ya sindano kwenye mshipa.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, maumivu ya tumbo, kutokwa na damu, usumbufu kwenye kifua, kuwashwa na athari za mzio.[2] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[2] Ni dawa ya rangi zenye kuakisi mwanga (fluorescent) inayojifunga kwenye kipokezi cha foleti (folate), ambayo mara nyingi hutokea kwa kiasi kikubwa katika saratani ya ovari.[2]
Pafolasianini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya matibabu nchini Marekani mwaka wa 2021.[1] Vijenzi vingine vilivyotumika sawa ni pamoja na methailini ya bluu (methylene blue), sodiamu ya fluoreseini (fluorescein sodium) na 5-ALA.[3]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Cytalux- pafolacianine injection injection". DailyMed. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 18 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>
tag; name "PI2022" defined multiple times with different content - ↑ 2.0 2.1 2.2 "Cytalux- pafolacianine injection injection". DailyMed. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 18 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Lauwerends, LJ; Abbasi, H; Bakker Schut, TC; Van Driel, PBAA; Hardillo, JAU; Santos, IP; Barroso, EM; Koljenović, S; Vahrmeijer, AL (Juni 2022). "The complementary value of intraoperative fluorescence imaging and Raman spectroscopy for cancer surgery: combining the incompatibles". European journal of nuclear medicine and molecular imaging. 49 (7): 2364–2376. doi:10.1007/s00259-022-05705-z. PMID 35102436.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)