Onyi Papa Jey

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Onyi Papa Jey (jina kamili Bernard Onyango Ranginya , alizaliwa 1982 Kiyembe, Wilaya ya Suba) ni muimbaji wa muziki wa mtindo wa ohangla nchini Kenya

Onyi Papa Jey alianza kucheza orutu akiwa katika shule ya msingi[1]. Alilazamika kukatiza masomo yake katika shule ya sekondari ya Tonga kwa kukosa karo[2]. Alijunga na bendi ya Tony Nyadundo mwaka wa 1999 na kutumbuiza naye mwaka wa 2002. Baadaye,alijiumga na kundi la wachezaji wa kitamaduni wa Nyamolo kwa muda. Pia,aliongoza bendi ya Langasta Stars mjini Eldoret kwa kipindi cha mwaka mmoja. Baadaye,alizuru pamoja na Jack Nyadundo (kakake mkubwa Tony Nyadundo) nchini Kenya na Tanzania. Akiwa Tanzania ,aliunda bendi za Super Suba na Koleko Newface. Aliondoka Tanzania baada ya miaka mitatu na kujiunga tena na kundi la wachezaji wa kitamaduni la Nyamolo kabla ya kujitenga kivyake[1][2].

Uinbaji wake ulipata umaarufu wa kitaaifa alipotoa album yake ya kwanza iliyoitwa "Raila ODM" na haswa wimbo wenyewe, alioutungia na uliohusu Raila Odinga, mgombezi wa urais wa chama cha Orange Democratic Movement kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2007 [1]. Onyi Papa Jey amekandarasiwa na kampuni ya SoundAfrica [2].

Aliteuliwa katika vitengo vitatu katika Tuzo za Muziki za Kisima za mwaka wa 2008 : Msanii wa Mwaka , Msanii bora wa kuchanganya utamaduni na usasa, na Wimbo wa Mwaka ("Raila ODM") [3]. Hata hivyo,hakushinda katikia kitengo chochote [4].

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Album zake:

  • Raila ODM
  • Mapatano

Marejeo[hariri | hariri chanzo]