Nenda kwa yaliyomo

Odiseo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Odiseo akirudi kwa Penelope baada ya miaka 20 ilhali hajatambuliwa bado (picha ya vigae, Ugiriki mnamo mwaka 450 KK)

Odiseo (gir. Ὀδυσεύς odise-ús, ing. Odysseus, pia kwa umbo la Kilatini Ulysses) ni mhusika mashuhuri katika masimulizi ya Mitholojia ya Kigiriki. Alikuwa mfalme wa kisiwa cha Ithaka, mume wa malkia Penelope na baba wa Telemachos. Anajulikana hasa kama mhusika muhimu katika utenzi wa Ilias na Odisei.

Katika masumilizi haya alishiriki katika vita ya Troia alipobuni "Farasi wa ubao" iliyowasaidia Wagiriki kushinda vita hii.

Safari yake ya kurudi nyumbani ilikuwa na matatizo mengi ikachukua miaka kumi alipopaswa kupambana na matatizo mengi na maadui wengi.

Hatimaye alifika nyumbani ambako watu hawakumtambua tena baada ya kukaa nke kwa miaka 20. Alikuta ikulu yake ilijaa wanaume wengi waliotaka kumwoa Penelope aliyetazamiwa kuwa mjane aliyepaswa kuolewa tena ili mume mpya apate mali yake na ufalme wa Ithaka. Hapa Odiseo alipigana nao akawashinda na kurudi katika ndoa na unyumba wake.

Masimulizi ya safari yake ya kurudi yanapatikana katika Utenzi wa Odisei (ing. Odyssey) ya mshairi Homeri ambayo ni kati ya mifano ya kale kabisa ya ushairi wa utamaduni wa Ulaya.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: