Nenda kwa yaliyomo

Nyani tatu wenye hekima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyani tatu wenye hekima kwenye hekalu huko Nikko, Japani

Nyani tatu wenye hekima ni picha au sanamu inayoonyesha nyani tatu wanafunika masikio, mdomo na macho kwa mikono yao. Maana yake ni "Kutosikia, kutosema na kutoona". Ni kipengee chenye asili katika maadili ya Japani na kiasili ni ushauri jinsi ya kushughulika mambo au maarifa mabaya kwa kutoyaangalia.

Inalingana na mafundisho ya Konfusio aliyesema: “Kile kisicholingani na sheria ya uzuri (= mwenendo ufaao), usikiangalie; kile ambacho hakiendani na sheria ya uzuri, usiisikilize; kile ambacho hakiendani na sheria ya uzuri, usizungumze juu yake; usifanye yasiyopatana na sheria ya uzuri."[1]

Baada ya kuenea katika pande nyingi za Dunia, inaeleweka pia kama ukosoaji wa msimamo wa kuvumilia ubaya[2][3].

  1. Confucian Analects, Kitabu cha 12, Wikisource, Chinese Cassics
  2. Searching for the fourth monkey in a corrupted world, gazeti la Nation (Bangkok), 21 Aprili 2011, iliangaliwa Septemba 2022
  3. How about monkey see, monkey DON’T do next time? , tovuti ya Winnipegfreepress.com ya tarehe 29.10.2011, iliangaliwa Septemba 2022