Nishati ya mwanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Nishati ya mwanga ni aina mojawapo ya nishati ambayo huchochea au huhamsha hisia ya kuona.

Nishati ni ule uwezo wa kuweza kufanya kazi. Kuna aina nyingine za nishati kama vile: nishati ya jua, nishati ya kikemikali, nishati ya nyuklia, nishati ya maji, nishati ya upepo na aina nyinginezo.

Kuna vyanzo vikuu vya nishati hiyo ambavyo ni vyanzo asili na vyanzo visivyo asili.

Vyanzo asili ni vyanzo ambavyo vina uwezo wa kutoa nishati vyenyewe bila kutegemea vyanzo vingine. Kwa mfano Jua, Kimetameta, Nyota na kadhalika.

Vyanzo visivyo asili ni vile vyanzo ambavyo haviwezi kutoa nishati vyenyewe, kama vile balbu, tochi na kadhalika.

Science.jpg Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nishati ya mwanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.