Nenda kwa yaliyomo

Ndege-mawingu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ndege-mawingu
Ndege-mawingu mkia-mweupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Phaethontiformes (Ndege kama ndege-mawingu)
Familia: Phaethontidae (Ndege walio na mnasaba na ndege-mawingu)
Jenasi: Phaethon
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Spishi 3:

Ndege-mawingu ni ndege wa bahari katika jenasi Phaethon, jenasi pekee ya familia Phaethontidae. Ndege hawa ni weupe na wana mileli mirefu katikati ya mkia. Hupitisha maisha yao yote baharini isipokuwa wakati wa majira ya kuzaa. Wanaweza kuogelea na kwa hivyo wana ngozi kati ya vidole; kwa kweli hawatembei vizuri. Huwakamata samaki na ngisi wakipiga mbizi au huwakamata panzi-bahari (samaki wanaoruka juu ya maji). Jike hutaga yai moja tu ndani ya tundu au mwanya wa mwamba visiwani kwa bahari.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]