Nenda kwa yaliyomo

Natasha Bacchus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Natasha "Courage" Bacchus (amezaliwa Toronto, 1977) ni mwanariadha wa kike kutoka Kanada ambaye ni kiziwi. Ameiwakilisha Kanada katika Michezo ya Majira ya Joto ya Viziwi ya 1993, 1997, na 2001.[1]

Bacchus amezaliwa na mama mwenye asii ya Guyana na ana mdogo wake wa kiume.[2] Alishinda medali 4 katika kazi yake ya Michezo ya Viziwi ambayo ilidumu kutoka 1993 hadi 2001, ikijumuisha medali 3 za dhahabu. Shirikisho la Michezo ya Viziwi la British Columbia lilimpa tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka kwa msimu wa 2014–2015.[3]

Baada ya kushindana katika michezo ya kimataifa,Bacchus alianza kufanya kazi kama mkufunzi binafsi.[4]

Bacchus pia amefuata kazi katika sanaa za maonyesho. Kazi zake kama mwigizaji ni pamoja na Destiny, USA (2019), The Black Drum (2019) katika nafasi ya Squib, na The Two Natashas (2020).[5][6]

Bacchus alionyesha kuunga mkono kwake hadharani kwa Black Lives Matter katika mkutano wa hadhara mnamo Juni 2020, akielezea uzoefu wake wa ubaguzi wa rangi kama mwanamke mweusi kiziwi. Anaunga mkono kuongezwa kwa upatikanaji wa mawasiliano kwa jamii ya viziwi katika mwingiliano wao na polisi.[7]

Katika mahojiano aliyofanya na NBC News alisema anapendelea zaidi kuitwa "Courage" kuliko Natasha.

  1. "Natasha Bacchus | Deaflympics". www.deaflympics.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2017-11-09.
  2. "I have faced rejection, discrimination and oppression, but I still keep going". Stir. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-10. Iliwekwa mnamo 2017-11-09.
  3. "Presenters". Red Dress Productions (kwa Kiingereza (Canada)). Iliwekwa mnamo 2020-10-16.
  4. "Presenters". Red Dress Productions (kwa Kiingereza (Canada)). Iliwekwa mnamo 2020-10-16.
  5. "Natasha Bacchus | The Toronto Theatre Database" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-10-15.
  6. "The Two Natashas". SOUND OFF (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-07. Iliwekwa mnamo 2020-10-15.
  7. "Deaf athlete Natasha Bacchus speaks out at Black Lives Matter rally". NBC News (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-10-15.