Nancy Kalembe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Nancy Kalembe
Alizaliwa 1980
Nchi Uganda
Kazi yake Mwanasiasa
Wazazi George Patrick Bageya na Cissy Kubaaza
Watoto 2

Nancy Linda Kalembe (alizaliwa mnamo mwaka 1980) ni mwanasiasa kutokea nchini Uganda.

Aligombea urais mnamo mwaka 2021, ambapo alikuwa mwanamke pekee kugombea, ila alishindwa na mpinzani wake Yoweri Museveni.

Maisha ya Awali naElimu[hariri | hariri chanzo]

Nancy Kalembe alizaliwa mwaka 1980 na kukulia katika wilaya ya Iganga nchini Uganda katika mkoa wa Busoga.[1][2][3] Alikuwa ni mmoja wa watoto kumi na nane katika familia yao na baba yake alikuwa akiitwa George Patrick Bageya aliekuwa mwanasiasa na mama yake aliitwa Cissy Kubaaza aliefariki wakati Nancy akiwa na umri wa miaka kumi na tatu.[2][3][4]

Kalembe alihitimu katika chuo kikuu cha Makerere mwaka 2017.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Kalembe aliolewa mwaka 2007, lakini baadae alikuja kutalikiana na mume wake, na katika kipindi cha ndoa yao walibahatika kupata watoto wawili.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nancy Kalembe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.