Nenda kwa yaliyomo

Mzingiro wa Yodfat

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kumbukumbu ya kisasa kwa watetezi wa Yodfat

Mzingiro wa Yodfat (kwa Kiebrania: יוֹדְפַת, pia Jotapata, Iotapata, Yodefat) ulikuwa mzingiro wa siku 47 na majeshi ya Dola la Roma dhidi ya mji wa Kiyahudi wa Yodfat uliotokea mwaka 67 BK, wakati wa Vita vya kwanza vya Kiyahudi. Uliongozwa na Jenerali wa Kirumi Vespasian na mwanae Titus, ambao baadaye walikuwa watawala wa Kirumi. Mzingiro ulimalizika na uvamizi wa mji, vifo vya wakazi wengi na utumwa wa wengine. Ulikuwa mapambano ya pili yenye umwagaji damu mwingi katika uasi huo, ukizidiwa tu na Mzingiro wa Yerusalemu, na muda mrefu zaidi isipokuwa Yerusalemu na Masada. Mzingiro huo uliandikwa na Josephus, ambaye alikuwa ameongoza majeshi ya Kiyahudi huko Yodfat na baadaye akakamatwa na Warumi.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Berlin, Andrea M.; Overman, J. Andrew (2004-01-14). The First Jewish Revolt: Archaeology, History and Ideology (kwa Kiingereza). Taylor & Francis. ISBN 978-0-203-16744-1.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mzingiro wa Yodfat kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.