Mwanaidi Mayowela
Mandhari
| Mwanaidi Mayowela | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Kazi yake | mjasiriamali |
Mwanaidi Mayowela ni mwanamke mjasiriamali ambaye hapo awali alikuwa anaombaomba maeneo ya posta kulingana na changamoto ya viungo vya mwili wake (ulemavu)[1].
Kwa kuona ni kwa jinsi gani anaweza kujikwamua kimaisha kwa kutumia mikono yake, mwanamke huyu ndipo akajiunga na kikundi cha wamama wenzie waliokua wanajishuhulisha na kazi za mikono.
Mwanaidi Mayowela pia alionesha nia ya kutaka kufanya biashara yoyote ambayo ingeweza kumsaidia, aliweza kuanza kutengeneza bangili za asili (utamaduni) pamoja na mikoba ambayo alikuwa anauzia maeneo yale aliyokuwa anaombaomba[2].
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Aprili 2017 alipata Tuzo ya heshima na katika tuzo za Malkia wa Nguvu zinazoratibiwa na Clouds Media Group na washirika wake.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu wasifu wa Mtanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |