Mussasa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mussasa alikuwa malkia wa Jaga katika karne ya 17.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Mussasa alikuwa mke wa Donji, gavana wa Matamba. Mussasa alijulikana kuwa shujaa mkali na hata kushindana na wanaume wa wakati wake.[1] Mara tu baada ya kifo cha Mfalme Zimbo, mume wa Mussasa, Donji, alianza kuchukua utawala wa majimbo jirani. Mussasa mara tu baada ya kifo cha mumewe, aliendeleza utawala na kuongeza eneo la ufalme wake.[1] Taifa lake lilikuwa kando ya mto Cunene katika eneo ambalo sasa ni Angola..[2] Alijenga ufalme wake kwa kiasi kikubwa kupitia jeshi lake, na kuongoza wanajeshi vitani. Mussasa alimfundisha binti yake Tembandumba kuwa mwanajeshi na kumchukua kwenda kupigana bega kwa bega vitani.[1] Tembandumba, ambaye alijipatia sifa ya kuwa mkali kama mama yake,[1] alimfuatia Mussasa kama malkia.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 Clayton, Ellen C. (1879). Female Warriors: memorials of female valour and heroism, from the mythological ages to the present era. Taylor and Co. uk. 190. 
  2. 2.0 2.1 "The Amazons: Chapter VII: Amazons of Africa". www.sacred-texts.com. Iliwekwa mnamo 2018-11-23. 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mussasa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.