Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Muddyb/MUM sw

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Habari zenu wana Wikipedia,

Katika kuunga mkono juhudi za Wikimedia Foundation kupitia kampeni ya Wikilove Africa, tunakuletea Edit-a-thon kupitia Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM) mnamo Oktoba 2024. Tukio hili la siku mbili litaandaliwa kwa lengo la kuongeza uelewa na ushiriki katika miradi ya Wikimedia, hasa Wikipedia.

Katika Edit-a-thon hii, tutatoa mafunzo kwa washiriki kuhusu:

  • Wikipedia ni nini: Historia ya Wikipedia, maadili yake, na umuhimu wake katika kutoa maarifa kwa umma kupitia mtandao.
  • Mwanzilishi wa Wikipedia: Historia ya kuanzishwa kwa Wikipedia na jinsi ilivyokua kuwa rasilimali muhimu duniani.
  • Jinsi ya Kushiriki: Mchakato wa kujiandikisha kama mchangiaji, kuhariri makala, kuchangia katika Wikipedia.
  • Mafunzo kwa Vitendo: Kuonyesha kwa vitendo jinsi ya kuwa sehemu ya jamii ya Wikipedia kwa njia rahisi na isiyo na changamoto.

Kwa kuongezea katika mafunzo ya jumla, tutajikita zaidi katika kuandika makala kuhusu Afrika, ikichukua maeneo ya msingi kama:

  • Afya: Makala juu ya mifumo ya utoaji huduma ya afya, magonjwa, na mipango inayohusu uendelezwaji wa sekta ya afya Afrika.
  • Elimu: Itatazamia mifumo na taasisi za elimu, sera, na mafanikio ya elimu ya Afrika.
  • Miundombinu: Maelezo ya kina juu ya usafirishaji, mawasiliano, na kazi zote zenye kuleta maendeleo kwa umma wote wa Afrika.
  • Siasa: Itatazamia mifumo ya kisiasas, viongozi, na matukio ya kihistoria ya mataifa ya Afrika.
  • Maendeleo: Ukaguaji wa maendeleo ya kiuchumi, misaada ya kimatafaifa, na ukuaji wa maendeleo barani Afrika.

Wawezeshaji na Walimu

[hariri | hariri chanzo]
  • Wawezeshaji: Muddyb, Iddy Ninga, na Aneth (au mtu mwingine yeyote anayefaa kama Aneth ratiba zake zitabadilika). Pia watakuwepo wanawakipedia ya Morogoro iwapo wakakti utawaruzuku.
  • Walimu: Watatu kutoka MUM (Watatoa mafunzo na usaidizi wakati wa mafunzo na mazoezi).

Hii ni mipango ya awali kwa ajili ya Edit-a-thon na itakuwa na manufaa kwa washiriki wote kwa kuimarisha uelewa wao na uwezo wa kuchangia kwenye Wikipedia. Ikiwa kuna maswali au maoni, tafadhali yachangie kwa ajili ya kuboresha mipango hii.

Ratiba ya Matukio

[hariri | hariri chanzo]
Muda Kipengele Maelezo
Siku ya 1 9:00 AM - 10:00 AM Utangulizi na Mafunzo ya Awali: Utangulizi kuhusu Wikipedia, historia yake, na jinsi inavyofanya kazi.
10:00 AM - 11:00 AM Mafunzo ya Kuunda Akaunti na Kuanzisha Makala: Mchakato wa kujiandikisha na kuanzisha makala mpya.
11:00 AM - 12:00 PM Mafunzo ya Kuongeza Maudhui na Marekebisho: Jinsi ya kuongeza maudhui na kufanya marekebisho kwenye makala zilizopo.
12:00 PM - 1:00 PM Muda wa Chakula cha Mchana
1:00 PM - 3:00 PM Mazoezi ya Vitendo: Washiriki watafanya mazoezi ya vitendo ya kuhariri na kuongeza maudhui kwenye Wikipedia.
3:00 PM - 4:00 PM Maswali na Majibu: Kipindi cha maswali na majibu ili kufafanua na kutoa msaada wa ziada.
Siku ya 2 9:00 AM - 10:00 AM Mafunzo ya Juu na Urekebishaji: Kupanua uelewa wa maelezo waliyojifunza na kufanya urekebishaji wa makala.
10:00 AM - 12:00 PM Kazi ya Kundi: Washiriki watagawanywa katika vikundi na kufanya kazi pamoja kuandika au kuboresha makala.
12:00 PM - 1:00 PM Muda wa Chakula cha Mchana
1:00 PM - 3:00 PM Kuendelea na Kazi ya Kundi na Uwasilishaji: Kazi ya kundi itaendelea na vikundi vitawasilisha matokeo yao.
3:00 PM - 4:00 PM Hitimisho na Tuzo: Hitimisho la mafunzo, utoaji wa tuzo kwa washindi, na tathmini ya tukio.
Bajeti ya EDITHON
[hariri | hariri chanzo]
Kipengele Maelezo Idadi Gharama (TZS) Jumla (TZS) Gharama (USD) Jumla (USD)
Chakula na Vinywaji Chakula na vinywaji kwa washiriki 31 31 30,000 930,000 $11.04 $342.13
Matangazo Mabango (Moja Nje na Moja Ndani) 2 230,000 460,000 $84.61 $169.23
Mawasiliano na Vifaa Handouts (Vipeperushi vya mafunzo) 40 3,000 120,000 $1.10 $44.15
Bidhaa za Kumbukumbu Fulana (T-shirts) kwa washiriki na waandaaji 31 25,000 775,000 $9.20 $285.11
Usafiri na Malazi Gharama za Usafiri na Malazi kwa Waandaaji wa Tukio 3 130,000 390,000 $47.83 $143.48
Zawadi na Tuzo Gharama za zawadi kwa wachangiaji 5 bora wa Wikipedia 5 100,000 500,000 $36.79 $183.94
Intaneti na Huduma Gharama za Intaneti kwa ajili ya uhariri - baada ya tukio 3 100,000 300,000 $36.79 $110.37
Vifaa na Zana Gharama za vifaa vya IT kama kamera, laptops na projector 1 500,000 500,000 $183.94 $183.94
Nyinginezo Gharama za dharura wakati wa tukio 1 100,000 100,000 $36.79 $36.79
Jumla 4,075,000 $1,449.14

Jumla ya Gharama:

[hariri | hariri chanzo]
  • Jumla ya Gharama (TZS): 4,075,000 TZS
  • Jumla ya Gharama (USD): $1,449.14.00 USD