Mtumiaji:Kaanaeli Kaale/Lucy Lyatuu
Kaanaeli Kaale/Lucy Lyatuu |
---|
Lucy Lyatuu (Alizaliwa Machi 14. 1977) ni mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania. anapenda kuandika habari za kijamii na mwaka huu ametia fora kwa kuandika habari kuhusu ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid 19).
Elimu yake
[hariri | hariri chanzo]Lucy alihitimu kidato cha nne mwaka 1995 katika sekondari ya Kidia. alihitimu kidato cha sita mwaka katika Sekondary ya Mkwawa mwaka 1998. Alipata stashahada ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ).
Habari kuhusu ugonjwa wa korona
[hariri | hariri chanzo]Lucy ameandika habari mbalimbali kuelimisha jamii kuhusu homa kali ya mapafu maarufu kama Korona ama kwa lugha ya kitaalam COVID 19 [1] Lucy ameandika maoni katika gazeti la Habari Leo kuhimiza umma wa Watanzania kuwafundisha na kuwahamasisha wanafunzi juu ya umuhimu wa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa korona.[2]
- ↑ Chuo Kikuu Dar es Salaam (2020). Elimika kuhusu ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya CORONA. https://www.udsm.ac.tz/web/index.php/announcements/elimika-kuhusu-ugonjwa-wa-homa-kali-ya-mapafu-unaosababishwa-na-virusi-vya-corona retrieved July 2, 2020
- ↑ https://habarileo.co.tz/habari/2020-06-215eef0bb94448f.aspx Lucy Lyatuu (Habari Leo 21 Juni 2020) Wanafunzi wahimizwe tahadhari ya Korona. Imetazamwa Julai 2, 2020