Mtumiaji:Hafidh Ame Sheha Pandu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hafidh Ame Sheha Pandu (amezaliwa 01 Januari, 1981) ni Mwalimu na Mtaalamu wa Afya, nchini Tanzania, Zanzibar. Alifahamika sana kwa uhusika wa "Baba" (2003) alioshiriki mashindano ya uigizaji akiwa mwanafunzi katika Chuo cha Ualimu Nkrumah (Beit-el-Ras) Bububu, Zanzibar. Hafidh alianza shule ya Msingi Muyuni, Unguja mwaka 1989, kisha baadaye kuhamia Skuli ya Haile Selassie iliyopo Vuga kwa ajili ya elimu ya Sekondari, baadaye akaenda Chuo cha Afya Mbweni (CHS) na kisha Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Tunguu, Zanzibar na kupata shada yake ya kwanza katika masomo ya Sayansi na Elimu. Hafidh amekua anasomesha masomo ya Sayansi katika skuli ya Msingi Kilimahewa "A" unguja.