Mto Ember
Mto Ember ni mto katika kata ya Surrey, Uingereza Ni tawimto la Mto Mole ambao unagawanyika mara mbili katika Hifadhi ya Kisiwa cha barn katika Kusini Mashariki na Magharibi Molesey. Sehemu kubwa huwa Mto Ember na hutiririka katika mashariki na kisha magharibi kuzunguka hifadhi. Mto Mole huelekea mashariki na kisha kaskazini kuzunguka hifadhi. Mito hii miwili kisha hutiririka kandd ya mwingine kuelekea upande wa kaskazini mashariki, na kuungna mita 400 kabla ya kujiunga na Mto Thames upande wa kusini juu ya Teddington Lock kando ya Ikulu ya Mahakama ya Hampton.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mto Mole uliwahi tririka kwenye Mto Thames pekee yake katioka pande za juu ambapo daraja la Mahakama ya Hamptonimevuka mto. Hata hivyo, mwanzo wa miaka ya 1930, wakati Mahakama ya Hampton na daraja ilijengwa, Mto Mole ulielekezwa kuungana na Ember na mito hii miwili sasa inajiuga na Thames katika mtaro moja mnene,ukiochukuliwa hapo awali na mto Ember. Kumekuwa na mabadiliko katika mikondo ya mito katika mito hii miwili katika mpango wa kuzuia mafuriko makubwa tangu mafuriko makubwa katika eneo hili mwaka wa 1947 na 1968.[1]
Kinu cha Ember kilisimama katika kisiwa katika Ember karibu na njia ya Mahakama ya Hampton. Hii inaweza kufikiwa kupitia daraja la mguu katika mwisho wa barabara ya Orchard. Kinu hiki kilibomolewa katika mwaka wa 1837 na maporomoko ya maji pande zote mbili ndiyo yamebaki kuashiria eneo hili. Kinu hiki hapo awali kilikuwa cha nafaka lakini baadaye kutumika kama kiwanda cha waya ya shaba na chuma. Sehemu hii ya Ember imepitiwa na mtaro mpya wa mpango wa a kuzuia mafuriko , lakini kuna maji kiasi katika mkondo wa awali ili kukaa kama unatumika.[2]
Uvuvi
[hariri | hariri chanzo]Kuna sehemu ya mto katika Old Cow Common, Molesey Mashariki ambapo kuna uvuvi bure wa kwa Pike (hadi 15 £ s), bream, carp, chub, Dace, sangara, Crow na rudd. [3]
Angalia pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Historia ya Molesey Mashariki". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-20. Iliwekwa mnamo 2010-01-28.
- ↑ Mwelekezo katika Viwanda vya Akiolojia vya Borough katika Elmbridge
- ↑ "mwelekezo wa maji safi". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-28. Iliwekwa mnamo 2010-01-28.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]51°23′34″N 0°21′23″W / 51.39272°N 0.35642°W
Makala hii kuhusu maeneo ya Uingereza bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Ember kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |