Nenda kwa yaliyomo

Morgunblaðið

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Morgunblaðið
Jina la gazeti Morgunblaðið
Aina ya gazeti Gazeti la kila sikuTangu mwaka wa 2003
Lilianzishwa 2 Novemba 1913
Eneo la kuchapishwa Iceland
Nchi Iceland
Mwanzilishi *. Vilhjálmur Finsen
*. Olaf Björnsson
Mhariri Davíð Oddsson mmoja wa timu ya wahariri
Mmiliki Kampuni ya Árvakur
Nakala zinazosambazwa 50,000 - 55,000 kila siku
Tovuti Tovuti Rasmi ya Morgunblaðið

Morgunblaðið (Swahili: Gazeti la Asubuhi) ni gazeti linalochapishwa katika nchi ya Iceland,lilianzishwa na Vilhjálmur Finsen & Olaf Björnsson. Toleo la kwanza lilikuwa na kurasa nane tu lilichapishwa tarehe 2 Novemba 1913. Miaka sita baadaye, katika mwaka wa 1919,shirika la Árvakur likanunua kampuni hiyo. Jarida hili lilikuwa na uhusiano wa karibu na chama cha Independence, hasa wakati wa Vita Baridi. Wahariri wake na wanaripoti wake wa bunge waliketi katika mikutano ya bunge mpaka mwaka wa 1983,wakati Mwenyekiti wa Bodi ya Árvakur alikuwa ,pia, Mwenyekiti wa chama cha Independence,Geir Hallgrímsson. Kulikuwa na uamuzi kuwa uhusiano huo haungesaidia chama au gazeti hilo kwa njia yoyote. Ingawa uhusiano na chama cha Independence sio wa moja kwa moja kama ule wa miongo iliyopita, jarida hili hukosolewa kwa kuegemea msimamo wa chama hicho hasa katika misimu ya uchaguzi. Jarida hili huwa na maadili ya kihafidhina sawa na yale ya chama cha Independence na limeonyesha msimamo huru katika masuala kadhaa muhimu kama mjadala kuhusu usambazaji wa haki za uvuvi. Hivi majuzi, gazeti hili limechukua hatua ya kuajiri wanahabari waliochukua msimamo wa kuegemea sera za kushoto na gazeti hili limeendeleza sera za kutetea haki za wanawake katika kurasa zake.

Tangu chapisho lake la hapo awali, Morgunblaðið halikuchapishwa Jumatatu lakini baada ya muda lilijiundia jina kama gazeti bora. Lilikuwa gazeti bora kabisa nchini Iceland siku nyingi huku likiongoza kabisa katika mwanzo wa miaka ya 1970 na likashinda magazeti mengine yote kwa mbali katika wakati huo.Miongo mitatu iliyofuata, gazeti hili liliongoza bila ushindani wowote mkali. Katika wakati huu wa mafanikio, Morgunblaðið lilianzisha sehemu maalum kuhusu fedha, uvuvi, vyakula na kadhalika. Baada ya usambazaji wa bure (magazeti yakiwasilishwa hadi nyumbani mwa watu), gazeti la Fréttablaðið lilileta ushindani kwa kuanzisha toleo la Jumatatu. Morgunblaðið likaitikia changamoto na tangu mwaka wa 2003 likachapishwa kila siku ya wiki, likiwa na kurasa mbalimbali kati ya kurasa 60 na kurasa 120. Matangazo huchukua asilimia 30 - asilimia 40 ya nafasi ya makala. Usambazaji wa nakala wa kila siku ni kati ya 50,000 na 55,000, nyingi za hizi zikiwa zimeagizwa na watu. Usambazaji hulenga zaidi eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo, hasa katika jiji kuu la Reykjavik.

Kama matokeo ya shida za kiuchumi za 2008 nchini Iceland, jarida la 24 stundir, linalochapishwa na Morgunblaðið, liliacha kuchapishwa mnamo 10 Oktoba 2008 na kusababisha wafanyikazi 20 kufutwa kazi.

Katika uamuzi wa utata ,wamiliki wa gazeti waliamua katika mwezi wa Septemba 2009 kuteua Davíð Oddsson , aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iceland kwa muda mrefu kabisa na alikuwa Mkuu wa zamani wa Benki Kuu, kama mmoja wa wahariri wa gazeti hilo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.mbl.is/mm/frettir/innlent/2009/09/24/david_og_haraldur_ritstjorar/ 24. Septemba 2009

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]