Mlima Jamimbi
Mandhari
Mlima Jamimbi (pia Chamembe) ni mrefu zaidi kati ya Milima ya Kipengere (kwa Kiingereza: "Kipengere Range" au "Livingstone Mountains") ambayo iko kusini magharibi mwa Tanzania kwenye ncha ya kaskazini ya Ziwa Malawi. Kama Mlima Mtorwe (m 2961) inahesabiwa kuwa sehemu ya Kipengere, Jamimbi ni mlima mkubwa wa pili.
Mlima Jamimbi uko 9° 41' S na unashuka moja kwa moja ziwani.
Kilele chake kiko mita 2,925 juu ya usawa wa bahari.