Nenda kwa yaliyomo

Mlima Abul Kasim

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mlima Abdul Kassim)

Mlima Abul Kasim ni mlima unaopatikana kusini mashariki mwa Ethiopia, eneo la Arsi katika ukanda wa Oromia. Mlima huo ndio sehemu yenye mwinuko mrefu zaidi katika Seru woreda, ukiwa na urefu wa mita 2573 juu ya usawa wa bahari. [1]

Mlima huo umekua na faida nyingi kwa wakazi waliopo karibu nao, hasa watu wa jamii ya Waoromo ambao huutumia kama sehemu yao ya utamaduni na dini (kuhiji), vilevile umekuwa ukitumiwa kama makumbusho ya kaburi la aliyekuwa mfuasi mkubwa wa dini ya Kiislamu nchini Ethiopia Mtakatifu Sheikh Hussein.

Trimingham huonesha kuwa kaburi limefunikwa kwa shanga za glasi na mapambo ya shaba. Baada ya shughuli za kitamaduni na kidini, mapambo hayo huchukuliwa kama vitu vitakatifu na huwekwa msituni kwenye miti; hivyo haitakiwi mgeni yeyote kujaribu kuyachukua wala kuyashika. "[2]

  1. http://130.238.24.99/library/resources/dossiers/local_history_of_ethiopia/A/ORTAA.pdf Ilihifadhiwa 28 Mei 2011 kwenye Wayback Machine. "Local History in Ethiopia"
  2. J. Spencer Trimingham, Islam in Ethiopia (Oxford: Geoffrey Cumberlege for the University Press, 1952), p. 255.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mlima Abul Kasim kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.