Mkoa wa Thies
Mandhari
Mkoa wa Thiès ni mkoa mmojawapo nchini Senegal. Makao makuu yako mjini Thiès. Mkoa una eneo la kilomita za mraba 6,670 linalokaliwa na wakazi 1,788,864 [1].
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Mkoa una maeneo mawili ya pwani, moja upande wa kaskazini kwenye Grande Côte (pwani kubwa) penye soko la mboga la Niayes, na moja upande wa kusini kwenye Petite Côte (pwani ndogo) ambayo ni moja ya maeneo ya kitalii ya Senegal.
Mkoa huu unazunguka Rasi ya Cap-Vert yenye mji mkuu Dakar, hivyo reli na barabara kuu za nchi zinapita mkoani.
Wilaya
[hariri | hariri chanzo]Mkoa wa Thiès umegawanywa katika wilaya 3 (departements):
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.citypopulation.de/en/senegal/admin/ Senegal: administrative divisions