Milima ya Mwezi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya ramani ya milima ya mwezi

Milima ya Mwezi ni jina la kihistoria kwa ajili ya safu ya milima ya Afrika ya Kati ambayo ni asili ya mto Nile. Milima hii ya mwezi ilitajwa katika maandiko ya Eratosthenes na Claudius Ptolemayo.

Kufuatana na "jiografia" ya Ptolemayo milima hii inapatikana upande wa magharibi wa Rhapta inayoaminiwa ilikuwepo kwenye pwani la Tanzania labda huko Pangani. "Kutoka hapa kuelekea magharibi iko milima ya mwezi. Maziwa ya mto Nile yanapokea maji yao kutoka theluji iliyopo juu ya milima hii."

Hakuna uhakika ni milima ipi ya leo. Katika historia milima ya Ethiopia, Kilimanjaro na milima ya Ruwenzori imeshatazamiwa kuwa milima ya mwezi ya kale.

Wataalamu wengi kidogo huelekea kukubali milima ya Ruwenzori. Milima hii iko karibu na maziwa makubwa ambako mto Nile unatoka; vilele vya juu vina theluji. Mlima wa Kilimanjaro una theluji lakini iko mbali na maziwa ya chanzo cha Nile. Milima ya Ethiopia peye asili ya Nile ya buluu haina theluji ya kudumu.

Zaidi ya hapo hakuna uhakika kwa sababu milima ya juu iko karibu na maziwa yote kwenye chanzo cha mto Nile.