Nenda kwa yaliyomo

Mikel Arteta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mikel Arteta

Mikel Arteta Amatriain (alizaliwa 26 Machi 1982[1]) ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu na sasa meneja wa klabu ya Arsenal.[2] Arteta alizaliwa San Sebastian, Hispania.

Arteta alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Barcelona mwaka 1999 lakini kutokana na kupata muda mfupi wa kucheza ulipelekea kuhamia Paris Saint-Germain kwa mkopo mnamo 2001. Alijiunga na Rangers mwaka 2002, ambapo alidumu kwa miaka miwili. 2004 alirudi Uhispania kuitumikia Real Sociedad. Alihamia Everton mwaka 2005 ambapo alidumu kwa miaka sita. 2011 alijiunga na Arsenal ambapo aliitumikia kwa miaka mitano hadi 2016 alipoamua kustaafu na kujiunga na ukufunzi na alianzia kama kocha msaidizi Manchester City (2016), na kuanzia Juni 2019, alijiunga rasmi Arsenal kama kocha mkuu.


  1. "2015/16 Player Shirt Numbers | Barclays Premier League". web.archive.org. 2015-08-09. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-08-09. Iliwekwa mnamo 2024-09-23.
  2. "Mikel Arteta: Overview". Premier League. Iliwekwa mnamo 3 Desemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mikel Arteta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.