Nenda kwa yaliyomo

Miguel Ángel Félix

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Miguel Ángel Félix
Amezaliwa Januari 8,1946
Bellavista
Nchi mexico
Kazi yake mlanguzi wa dawa za kulevya

Miguel Ángel Félix Gallardo (alizaliwa Januari 8, 1946) kawaida akijulikana na washirika wake kwa jina la El Jefe de Jefes ("Bosi wa Mabosi") na pia El Padrino ("Godfather", kwa Kiswahili "Msimamizi (wa ubatizo)") ni mlanguzi wa dawa za kulevya wa Mexiko na aliwahi kuhukumiwa na jeShi la polisi Mexico. AlikuWa ni mmoja wa waanzilishi wa Guadalajara Cartel (ngome ya utawala) mnamo miaka ya 1970s. Katika miaka ya 1980, Guadalajara Cartel ilitawala au thibiti asilimia kubwa ya ulanguzi wa madawa ya kulevya huko Mexico na katika mipaka ya Marekani na Mexiko.

Félix Gallardo alikamatwa na kuwekwa kizuizini mwaka 1989 kwa kosa la jinai la mauaji ya wakala aitwaye Enrique "Kiki" Camarena wa kikosi cha Drug Enforcement Administration (DEA) shirika la kuzuia ulanguzi wa madawa ya kulevya. Alitumikia miaka arobaini (40) katika jela la Altiplano maximum-security prison (Gereza lenye usalama wa hali ya juu) na aliweza kuhamishwa kwenye Gereza la kizuizi wa kati mwaka 2014 kwasababu ya hali yake ya kiafya.

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

kuzaliwa kwake katika ranchi huko Bellavista, nje ya Culiacán, Sinaloa, Félix Gallardo alihitimu shule yake ya sekondari na kusomea biashara alipofika chuo. Alipata kazi ya uwakala wa polisi wa mahakama huko Mexico (Federal Judicial Police.[1]Na alifanya kazi kama mlinzi wa familia ya Gavana wa mji wa Sinaloa aliejulikana kwa jina Leopoldo Sánchez Celis, ambaye aliyemsaidia Félix Gallardo kutengeneza shirika lake la ulanguzi wa madawa ya kulevya. Na pia alikua Godfather wa mtoto wake Sánchez Celis, aitwaye Rodolfo.[2][3][4]

Félix Gallardo alianza kazi kwa walanguzi wa madawa ya kulevya, udalali wa rushwa kwa viongozi wa nchi, akiwa pamoja na Rafael Caro Quintero na Ernesto Fonseca Carrillo, ambao wote walikua wakifanya kazi kwenye shirika la uhalifu la Avilés, na baadae kuchukua uongozi au utawala barabara zote za ulanguzi baada ya Avilés kufariki kwenye majibizano ya risasi na askari.

  1. Astorga, Luis (1999); "Cocaine in Mexico: A Prelude to 'los Narcos'" in Gootenberg, Paul (ed.) Cocaine: Global Histories; Routledge; p. 187
  2. Malcolm Beith (2010). The last narco. Internet Archive. Grove Press. ISBN 978-0-8021-1952-0.
  3. Kenny, Paul; Serrano, Monica; Sotomayor, Arturo C. (2013-06-17). Mexico's Security Failure: Collapse into Criminal Violence (kwa Kiingereza). Routledge. ISBN 978-1-136-65050-5.
  4. Warner, Judith Ann (2010). U.S. Border Security: A Reference Handbook (kwa Kiingereza). ABC-CLIO. ISBN 978-1-59884-407-8.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Miguel Ángel Félix kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.