Michael Mokongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Michael Benoît Mokongo (alizaliwa tarehe 11 Julai 1986) ni mchezaji wa mpira wa kikapu ambaye mara ya mwisho alichezea AS Monaco Basket ya LNB Pro B nchini Ufaransa.[1]

Wasifu kitamaifa[hariri | hariri chanzo]

Kwa mara ya kwanza Mokongo aliwakilisha timu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kimataifa mwaka 2009 kwanye mashindano ya kufuzu AfroBasket. Alicheza AfroBasket mwaka 2011 akiwa na wastani wa pointi 11 na asisti 6. Pia Mokongo aliwahi kuichezea timu Ufaransa siku za nyuma, akiichezea katika Mashindano ya FIBA Europe mwaka 2006 timu ya watoto chini ya umri wa miaka 20. Awali alitarajiwa kuchezea Jamhuri ya Afrika ya Kati katika AfroBasket 2015 chini ya kocha mkuu Aubin-Thierry Goporo, lakini jeraha la goti lilimlazimu kutoshiriki mashindano hayo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Eurobasket. "Michael Mokongo Player Profile, ESC Trappes Saint Quentin Yvelines, News, Stats - Eurobasket". Eurobasket LLC. Iliwekwa mnamo 2022-09-02.