Michael Cardei

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mihaela Cardei ni mwanasayansi wa kompyuta nchini Marekani mwenye asili ya Romania anayejulikana sana kwa utafiti wake kuhusu mtandao wa matangazo ya pasiwaya. Ni profesa katika idara ya kompyuta na uhandisi wa Umeme na Sayansi ya Kompyuta katika chuo kikuu cha Florida Atlantic.[1]

Elimu na Taaluma[hariri | hariri chanzo]

Cardei alipata shahada ya kwanza katika sayansi ya Kompyuta mwaka 1995 na uzamili katika sayansi ya Kompyuta mwaka 1996, Katika Chuo Kikuu cha Politehnica cha Bucharest. Alimaliza Ph.D mwaka 2003 katika Chuo Kikuu cha Minnesota akiwa chini ya usimamizi wa Ding-Zhu Du.[2][3]

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Florida Atlantic kama Profesa msaidizi mnamo mwaka 2003, alipandishwa cheo na kuwa Profesa Mwaka 2014.[4]

Utambuzi[hariri | hariri chanzo]

Alitajwa na Chuo kikuu cha Florida Atlantic kuwa mtafiti bora wa mwaka katika ngazi ya profesa msaidizi kwa mwaka 2006-2007

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Mihaela Cardei". Florida Atlantic University (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-08-16. 
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-21. Iliwekwa mnamo 2022-08-16. 
  3. https://mathgenealogy.org/id.php?id=171936
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-21. Iliwekwa mnamo 2022-08-16.