Nenda kwa yaliyomo

Max Aarons

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aarons akipasha misuli joto upande Norwich city mwaka 2021

Maximillian James Aarons (alizaliwa 4 Januari 2000) ni raia wa Uingereza anayecheza kandanda la kulipwa kwenye nafasi ya beki wa kulia katika klabu ya AFC Bournemouth inacho shiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Maisha kwenye Klabu

[hariri | hariri chanzo]

Norwich City

[hariri | hariri chanzo]

Aarons alianza safari yake ya kandanda kwenye klabu ya Luton Town, mwaka 2016 aliamia na kujiunga kwenye timu ya vijana ya Norwich City.[1] Alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumiakia klabu ya Canaries mwezi wa 6 mwaka 2018,[2] majukumu yake yalianza kwenye kombe la EFL mchezo dhidi ya Stevenage tarehe 14 mwezi wa 8.[3] Alifunga goli lake la kwanza kwenye kombe la EFL, wiki mbili mbele ambapo alifunga goli la mwisho kwenye ushindi wa 3 – 1 dhidi ya Cardiff city. [4]Aarons alicheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu tarehe 2 mwezi wa 9, alianza kwenye East Anglian derby dhidi ya Ipswich Town, mchezo ulioisha kwa sare ya 1-1.[5] Tarehe 10 mwezi 10 aliongeza mkataba wa kuitumikia klabu iyo mpaka mwezi wa 6 mwaka 2023.[6]

Mwezi wa 4 mwaka 2021 Aarons alijumuishwa kwenye kikosi bora cha msimu ligi ya daraja la kwanza,[7] pia alishinda tuzo kama mchezaji kijana wa msimu 2018-19 EFL.[8] Alipanda daraja kushiriki ligi kuu nchini Uingereza na Norwich baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Blackburn Rovers.[9]

AFC Bournemouth

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 10 mwezi wa 8 mwaka 2023, Aarons alihamia AFC Bournemouth kwa ada ya paundi millioni 7.[10] Alicheza mchezo kwanza wa ligi kuu nchini Uingereza dhidi ya West Ham United mchezo ulioisha kwa sare ya 1-1.[11]

Majukumu kwenye timu ya Taifa

[hariri | hariri chanzo]

Msimu wa 2018-19 alijumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Uingereza vijana chini ya miaka 19 Septemba 2018.[12]

Tarehe 30 Agosti 2019, kwa mara ya kwanza Aarons alijumuishwa kwenye kikosi cha vijana chini miaka 21.[13]

  1. "Max Aarons signs first professional contract". Norwich City (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-26.
  2. "Max Aarons signs first professional contract". Norwich City (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-26.
  3. "Norwich City vs Stevenage on 14 Aug 18 - Match Centre - Norwich City". web.archive.org. 2018-09-16. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-16. Iliwekwa mnamo 2024-07-26.{{cite web}}: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
  4. "Cardiff City vs Norwich City on 28 Aug 18 - Match Centre - Norwich City". web.archive.org. 2018-09-16. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-16. Iliwekwa mnamo 2024-07-26.{{cite web}}: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
  5. "Ipswich Town vs Norwich City on 02 Sep 18 - Match Centre - Norwich City". web.archive.org. 2018-09-16. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-16. Iliwekwa mnamo 2024-07-26.{{cite web}}: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
  6. "Max Aarons rewarded with new deal at Norwich City". Norwich City (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-26.
  7. "EFL awards: Che Adams, Teemu Pukki & Billy Sharp on Championship shortlist", BBC Sport (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2019-03-26, iliwekwa mnamo 2024-07-26
  8. https://mobile.twitter.com/EFL/status/1115006671137509381
  9. "Norwich City 2-1 Blackburn Rovers: Canaries promoted after Stiepermann & Vrancic goals", BBC Sport (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2019-04-26, iliwekwa mnamo 2024-07-26
  10. www.afcb.co.uk https://www.afcb.co.uk/news/first-team/max-aarons-joins-the-cherries/. Iliwekwa mnamo 2024-07-26. {{cite web}}: Missing or empty |title= (help)
  11. https://www.skysports.com/football/news/11685/12937477/bournemouth-1-1-west-ham-dominic-solanke-rescues-point-for-cherries-after-jarrod-bowens-stunning-opener
  12. "England calling for Max Aarons". Eastern Daily Press (kwa Kiingereza). 2018-08-31. Iliwekwa mnamo 2024-07-26.
  13. The Football Association. "England U21s kick-off a new campaign and Aidy Boothroyd has picked his squad". www.thefa.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-26.