Marko Livaja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marko Livaja

Marko Livaja (alizaliwa 26 Agosti 1993) ni mchezaji wa Timu ya taifa ya kroatia ambaye anacheza katika klabu ya Kigiriki iitwayo AEK Athens iiliyopo katika Super League.

Kazi ya klabu[hariri | hariri chanzo]

Atalanta[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 31 Januari 2013 Livaja alikopwa katika klabu ya Atalanta akitoka katika klabu ya Inter Livaja alicheza kwa mara ya kwanza katika klabu hiyo dhidi ya Catania Calcio tarehe 10 Februari 2013 na alifunga goli lake la kwanza katika mechi dhidi ya A.S. Roma. Mnamo Aprili, Livaja alipewa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi katika klabu ya Atalanta Februari 2013 na mashabiki wa klabu hiyo. Tarehe 7 Mei, kabla ya mechi dhidi ya Juventus, Livaja mara nyingine alifukuzwa katika kikosi kutokana na uvunjaji wa nidhamu.

Rubin Kazan[hariri | hariri chanzo]

Livaja alisajiliwa na klabu ya Rubin Kazan tarehe 15 Mei 2014 juu ya mkataba wa miaka mitano. Mnamo tarehe 31 Agosti 2015, Rubin Kazan wanamuuza kwa mkopo katika Serie A katika klabu ya Empoli.Livaja alifunga mara moja tu katika mechi ya 18 mnamo Novemba 22 wakati wa mechi ambayo walisuluhu 2-2 dhidi ya Fiorentina.

Las Palmas[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 14 Julai 2016, Livaja alijiunga na La Liga katika klabu ya Las Palmas na kusaini mkataba hadi Juni 2020. Alicheza kwa mara ya kwanza tarehe 22 Agosti, alisaidia klabu yake ya Las Palmas katika ushindi dhidi ya Valencia 4-2.

Mnamo 4 Desemba 2016, alisaidia timu yake kwenye katika sare ya 1-1 dhidi ya Deportivo Alavés.Livaja alicheza mechi yake ya kwanza ya Copa del Rey mnamo tarehe 10 Januari mzunguko wa 16 dhidi ya Atlético Madrid, akifunga goli katika ushindi wa 2-3.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marko Livaja kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.