Nenda kwa yaliyomo

Marie Sanderson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Marie Elizabeth Sanderson alikuwa mwanageografia na climatologist wa Canada.[1][2][3][4]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Marie Lustig alizaliwa tarehe 16 Novemba 1921 huko Chesley, Ontario, Canada.[1] Alikuwa mmoja wa wahitimu wa kwanza katika geografia kutoka Chuo Kikuu cha Toronto, na kisha akapata shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Maryland na Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Michigan.[4]

Sanderson alisoma na C. W. Thornthwaite wakati aliokuwa akisomea shahada yake ya Uzamili, na mwaka 1949 alianzisha vifaa vya evapotranspirometers alivyovumbua kama sehemu ya jaribio la kwanza la hali ya hewa katika Northwest Territories, huko Norman Wells.[1]

Aliandika maisha ya walimu wake Griffith Taylor na C. W. Thornthwaite, na alichapisha vitabu kadhaa kuhusu maji na hali ya hewa.[1]


Maisha Binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2009, Sanderson alijichapishia mwenyewe kitabu chake cha kumbukumbu: High heels in the tundra : maisha yangu kama mtaalamu wa jiografia na mwanaharakati wa hali ya hewa".[5]

Ingawa alisafiri sehemu mbalimbali, Sanderson alitamka kwamba "mahali pendwa duniani kwake" ilikuwa Inverhuron kwenye Ziwa Huron ambapo alikuwa na nyumba ya mapumziko.[1]

Sanderson alifariki dunia kutokana na saratani ya matiti tarehe 12 Julai 2010, akiacha nyuma mabinti wawili, mwana, watoto wawili wa kambo, na wajukuu kumi.[1][6]

Hifadhi ya nyaraka za Sanderson inashikiliwa na Chuo Kikuu cha Wilfrid Laurier.[7]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marie Sanderson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 Howarth, Philip (Machi 2011). "Marie Sanderson (1921-2010)" (PDF). Arctic. 64 (1): 123-124. doi:10.14430/arctic4090. Iliwekwa mnamo 27 Juni 2022.
  2. "Marie Sanderson research team, Nunavut". images.ourontario.ca (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-05-27. Iliwekwa mnamo 27 Juni 2022. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  3. "Alumni of note". exhibitions.lib.umd.edu. University of Maryland. Iliwekwa mnamo 27 Juni 2022.
  4. 4.0 4.1 "Marie SANDERSON Obituary (2010) The Globe and Mail". Legacy.com. Iliwekwa mnamo 27 Juni 2022.
  5. Andrey, Jean (Machi 2011). "High Heels in the Tundra: My Life as a Geographer and Climatologist by Marie Sanderson". The Canadian Geographer / Le Géographe canadien. 55 (1): 127–128. doi:10.1111/j.1541-0064.2010.00350.x. Pia inapatikana mtandaoni
  6. "Mtunukiwa wa shahada ya heshima afariki | UNews", www.ulethbridge.ca, 12 Agosti 2010. (en) 
  7. "Finding Aid - Marie Sanderson fonds (S703)" (PDF). Chuo Kikuu cha Wilfrid Laurier. 2019. Iliwekwa mnamo 27 Juni 2022.